NI WAKATI WA MAAMUZI TOKA KWA VIONGOZI WETU NA SISI WENYEWE. - PARACHUKA

Friday, June 21, 2013

NI WAKATI WA MAAMUZI TOKA KWA VIONGOZI WETU NA SISI WENYEWE.

 Tunapozungumzia amani tuna maanisha hali ya utulivu katika hali zote za ndani ya nafsi ya mtu mpaka nje kwenye mwonekano wa kawaida, amani si kula na kulala tu tukasema amani ipo amani NI WAKATI WA MAAMUZI TOKA KWA VIONGOZI WETU NA SISI WENYEWE.ni ule uhuru wa kuweza kuongelea mambo bila kujifichaficha kama ilivyo kwa baadhi ya watu. Amani ni kuwa huru, uhuru usiofungwa na kukanda mizwa kwa namna yoyote ila amani inakuwa ndani ya mipaka ya sheria maanasheria ndo mpaka na  ulinzi kwa kika mwanadamu, amani ya kutokuwa na vita alafu tunajisifia tuna amani ni UNAFKI wa halli ya juu, amani ni zaidi ya kutokuwa na vita. mfano Tanzania haina vita ila haina amani, machafuko yanayotokea mara kwa mara ndani ya nchi hatwezi kujisifia amani ya kweli tunayo. Muda umefika wa kutafuta amani ya kweli. ninani atakayeleta amani ya kweli? ni swali ila amani inaletwa na viongozi wa nchi wakisaidiana na raia wote.
Je serikali ipo tayari kuleta amani kama nchi ya Sweeden? Tujiulize ninani kituvu cha amani ya nchi, Ndio rai ndo kitovu cha amani ya nchi ila bila viongozi wa nchi kuweka sheria ambazo zitatuongoza na kutuwekea mipaka hatwezi kufikia malengo ya amani tunayoiimba tunayo.
Amani lazima ilindwe kwa nguvu zote, pia kwa gharama ili iwepo sikuzote ndani ya nchi. Libya ilipoteza amani yao ya mwanzo ila kwasasa hawana hata amani iliyo kidogo wao wamekuwa watu wa kusikia wenzao wakizungumza kuhusu amani ila amani tena hawana.

Tanzania inawaza kuwa nchi ya kilamtu ka amani itakuwa wimbo vinywani mwa Watanzania,kiuchumi itapanda kwa kasi ya zaidi.

Nijukumu la viongozi walio katika sekta ya kutunza amani kuwa makini na kutoa fursa ya wanachi kuolezea hisisa zao juu ya malalamiko fulani kwa malengo ya kujenga hata kama yanakuwa hayakufurahishi kikubwa si kufurahishana, kikubwa ni kujenga nchi katika mstakabali wa amani, upendo, furaha na maridhiano.
Kwa ushauri ningependa kuona serikali inakuwa kali kwa wote wanaotaka kuvunja amani ya nchi pia yenyewe isiwe yakwanza kuvunja amani kwa maslahi ya kikundi fulani yote yakitimizwa natumaini amani aloiacha baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere itarejea kama mwanzo na maswala ya choko choka zinazotokea hapa nchini zitatowoka.
MUNGU ibariki TANZANIA, MUNGU ibarikia AFRIKA.

No comments:

Post a Comment