Tatizo la nguvu za kiume ni nini hasa? ni hali ya mwanaume
kushindwa kushiriki tendo la ndoa na mwenzi wake hasa kutokana na kiungo
chake(uume) kukosa nguvu au uwezo wa kufanikisha tendo hilo hasa kuanza ama
kumaliza, kwa maana nyingine tunaweza sema ni ile hali ya mwanaume kushindwa
kushiriki tendo la ndoa ipasavyo kutokana na ulegevu wa misuli ya uume. Kwa
kawaida inapaswa mwanaume kuwa na uwezo wa kuanza tendo la ndoa na mwenzi wake
na kuwa na ule uwezo wa kumaliza kwa muda unaozidi japo hata dakika tano kwa
raund ya kwanza, sasa kunawatu ambao akisha enda raundi moja anakuwa hana uwezo
tena wa kurudia, pia wengine unakuta amefikia hatua ambapo uume hauwezi
kusimama kabisa labda mwanamke atumie nguvu nyingi sana kuweza kuupatia uhai.
Maranyingi wanaume wengi wanakumbwa na matatizo haya katika njia mbili kuu yani
msongo wa mawazo/maisha na matatizo mengine yanayohusiana na maisha, pia tatizo
jingine kubwa ndo hilo la kulegea kwa misuli ya uume ambayo ndo tunaita ukosefu
wa nguvu za kiume haswa.
Ukosefu wa nguvu wa kiume kusababishwako na changamoto za maisha ni rahisi zaidi kuoondokana nako maana unahitaji kufahamu hasa tatizo lipo wapi katika maisha na ukatatua hiyo changamoto alafu tatizo likawa limeisha kama sivyo ni kuweka akili sawa wakati uendapo kushiriki tendo la ndoa maana tendo la ndoa linahitaji utulivu wa akili zaidi
Ukosefu wa nguvu za kiume kusababishwako na kulegea kwa misuli ya uume.
hili ndilo tatizo haswa maana lazima tujue kwanini misuli ya uume inalegea? kwanza nitagusia sababu chache kwa juu juu ambazo ni uendeshaji wa baiskeli kwa muda mrefu, uendeshaji wa piki piki kwa muda mrefu , lishe isiyokidhi mahitaji ya mwili, baadhi ya michezo na mazoezi magumu na zaidi ya uwezo wa mwili, lishe duni, kukosa muda wa kupumzika wa kutosha, pia kuna baadhi ya magonjwa husababisha tatizo la nguvu za kiume mfano kisukari
Matatizo yasababishwayo na ukosefu wa nguvu za kiume ni mengi hasa katika familia, miongoni mwa matatizo hayo ni kuvunjika kwa ndoa, mwanaume kuwa mwoga hasa kushiriki tendo la ndoa na mwenzi wake maana anajua akishiriki tuu atatolewa knockout, watu kutumia fedha nyingi kujitibia tatizo hili pasipo mafanikio kutokana na dawa na maelekezo mabovu ya wanaojiita wataalamu na waganga, ufanisi mbovu wa kazi na majukumu ya kiuchumi na kijamii maana mtu akiwa na tatizo limsumbualo kichwa si rahisi kufanya majukumu yake vile impasavyo.
Suluhisho la ukosefu wa nguvu za kiume
- Jambo la kwanza kabisa ni kuyaepuka yale yote
yasababishayo misuli kulegea ka nilivyoelekeza hapo juu
- kupunguza mawazo maana msongo unafanya ufanisi unapotea
na unaonekana ka unatatizo la ulegevu wa misuli
- kula vyakula vyenu virutubisho vyote ila zingatia
vyakule vyenye protein kwa wingi zaid ya wanga na sukari maana protein
inajenga mwili na kurekebisha sehemu zilizoharibika.
- kumzika kwa muda wa kutosha hasa kulala.
- kingine na kwa msaada zaidi kwa wale wenye tatizo hasa
la ulegevu wa misuli ya uume ni kufanya mazoezi mara kwa mara hasa ya
kegel ambayo husaidia sana kurudisha uimara wa misuli.ukitaka namna ya
kufanya mazoezi hayo tafadhali soma makala yangu ya nyuma iliyoandikwa
(rudisha nguvu zako bila madhara)
Natumai makala hii itakuwa msaada na mkombozi kwa wengi, pia ni
vyema pindi upatapo matatizo ka haya ukamwone daktari kwa uchunguzi zaidi maana
unaweza kuona tatizo ni nguvu za kiume ila kumbe yawezekana kunatatizo jingine
lipo pembeni. kutokana na uchunguzi wa kidaktari anaweza kubaini tatizo liko
wapi na akakupatia matibabua ama ushauri wa kitabibu zaidi.
Nice
ReplyDelete