NAMNA BORA YA KUACHANA NA MPENZI WAKO. - PARACHUKA

Friday, December 14, 2012

NAMNA BORA YA KUACHANA NA MPENZI WAKO.


KUNA wakati kwenye mapenzi, inafikia hatua mtu akahisi amemchoka mpenzi wake. Kuna mambo mengi, lakini kubwa ni kwamba, anajikuta ameanza kufikiria kwamba, kumbe mwenzi aliye naye si sahihi kwake na hataki tena kuendelea naye.

 Katika uhusiano ambao bado si rasmi yaani ndoa loolote laweza kutokea, mfano katika kipindi cha uchumba hapa ndipo mahala mtu anapaswa kufanya maamuzi sahihi na yaliyo magumu maana hapa hanaonesha hatima yake ya mbele



Hili ni jambo la kawaida kwenye uhusiano. Rafiki zangu, angalizo moja muhimu katika mada hii ni kwamba, wale ambao tayari wapo kwenye ndoa, mada hii haiwahusu kabisa. Hapa nazungumza na walio kwenye uhusiano wa kimapenzi (pengine hata kwenye uchumba hawajafika).

Mapenzi ni hisia za ndani, uamuzi wa kuendelea na mtu katika hatua ya uchumba ambayo huambatana na ndoa ni uamuzi wa ndani wa mhusika mwenyewe. Hakuna wa kumshikia fimbo kumlazimisha.
Mnapokuwa kwenye uhusiano ni kipindi chenu cha kuchunguzana sana. Kila mmoja lazima amjue mwenzake sawasawa, hii itamsaidia kila mmoja kufahamu anakwenda kuingia kwenye ndoa na mtu wa aina gani.


Hapa nazungumzia eneo la KUACHANA. Ni kweli, umegundua kwamba hakufai (kwa sababu zako binafsi) ambazo kwa hakika huwezi kumweleza, lakini mwenzako ndiyo kwanza anaonekana amefika – hafikirii kuachana na wewe.
Inawezekana umejaribu kupima sababu zako na ukagundua ni za ‘kijinga’ ambazo huwezi kumwambia mpenzi wako, lakini MOYO wako umekuthibitishia kwamba huyo si CHAGUA lako na uking’ang’ania kuendelea naye basi FURAHA katika maisha yako itakuwa ni sawa na kitendawili kigumu mno.
KWANINI UNATAKA KUMWACHA?
Hii ni hatua ya kwanza rafiki yangu. Lazima ujiulize, ni kwa nini unataka kumwacha? Kama nilivyosema awali, ni vyema kuuchunguza moyo wako, maana isije ukamwacha kwa sababu ya tamaa zako au umeleweshwa kimapenzi na mwingine, ukashawishika kwa nje – baadaye utajuta.
Sababu kubwa ya kuachana kwenu inatakiwa iwe ile ya kutafuta amani ya moyo wako, maana umeshajichunguza na umegundua kwamba, kulazimisha kuendelea naye, maana yake utaishi maisha yasiyo na amani.
Kama ndivyo, wazo hili ni sahihi, lakini kumbuka hutakiwi kumwumiza mwenzako wakati ukitekeleza jambo hili ambalo ni matakwa yako binafsi.
SABABU ZINAZUNGUMZIKA?
Zipo sababu kuu mbili za kutaka kusitiza uhusiano. Ya kwanza nilishaifafanua kwenye kipengele kilichotangulia, lakini ya pili sasa ni kama kweli ana kasoro ambazo unaweza kumweleza moja kwa moja.
Kumbuka njia nitakazokufundisha hapa ni za muda mrefu, zinahitaji ufundi na inategemea na namna mwenzako atakavyopokea, hivyo kama unajua mwenzako hajatulia na ushahidi unao, mwekee mezani kuliko kumzungusha.
Ikiwa kipengele hiki hakikuhusu, basi twende wote hatua kwa hatua katika vipengele vifuatavyo;
PUNGUZA MAWASILIANO
Silaha ya kwanza ya mapenzi ni mawasiliano. Kuwasiliana ndipo kunapodumisha penzi. Hili lilikuwepo toka enzi na enzi, ingawa kwa sasa kuna maendeleo ya utandawazi, mawasiliano yamekuwa rahisi zaidi.
Punguza kumpigia simu, kumwandikia meseji au waraka pepe. Akikupigia yeye pokea, akituma meseji unaweza kujibu na wakati mwingine kuacha. Akikuuliza, mwambie una mambo mengi. Hii ni alama ya kwanza itakayomfanya ahisi uhusiano wenu umeanza kuyumba.

Hizi njia tutaendelea kujuzan kidogo kidogo mpaka ziishe
ANGALIZO:
Mi siamasishi watu kutengana ila naweka wazi mbinu ambazo ni sahihii katika kutengua uhusiano ambao unaonekana hauna tija kwa maisha ya mbeleni. maana si kila mchumba anafaa kuwa mume ama mke na ndo maana watu wanapitia uchumba ili kuchunguzana na kutafuta mtu anaekufaa sasa kama hakufai na hakidhi  malengo yako au vigezo ulivyojiwekea nikuachana nae na si kung'ang'ania.
kwaleo tuishie hapa ila tufuatilianane katika makala inayofuata.

No comments:

Post a Comment