JEREMY WUITSCHICK, kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 13 kutoka
Jimbo la Washington, Marekani, amepongezwa kwa kuweza kushika usukani wa
basi la shule na kuliongoza baada ya dreva wake kuzimia Jumatatu wiki
hii.
Kijana huyo alionekana kwenye video za kunasa matukio (CCTV)
akiliendesha basi hilo hadi sehemu salama na kisha kuzima injini yake
baada ya kuanza kwenda mrama katika viunga vya mji wa Tacoma.
Wakati akilisimamisha basi hilo, ofisa mmoja wa shule ambaye alikuwa
anashuhudia tukio hilo, alifika na kutoa huduma ya kumrudishia fahamu
dreva huyo. Vilevile, polisi walifika hapo na kuwaondoa wanafunzi 12
waliokuwa katika basi hilo.
No comments:
Post a Comment