Elimu ni msingi wa wanadamu na inawapa mwongozo mzuri wa leo na kesho, nukuu ya baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema msingi wa mtanzania ni elimu na elimu ndo inatengeneza mtanzania aliye bora. Jambo linalonishangaza ni matokeo ya wanafunzi wa kidato cha nne wa mwaka 2012 ambayo yalikuwa si mazuri na serikali ikaamua kuingilia kati ili kujaribu kuokoa jahazi japo hawakufanikiwa kwa asilimia mia.Wasiwasi umetanda ama unatanda baada ya wizara ya elimu kuamua kuongeza madaraja ya ufaulu, kutoka daraja la nne mpaka la tano( division ya kwanza mpaka ya tano) haya ni maamuzi ya wizara ya elimu ila mi ninamashaka sana na maamuzi yaliyo chukuliwa maana kinachoonekana ni kuokoa wanafunzi wengi wasipate sifuri ila swali je hao wanafunzi wanauwezo? au elimu inataka kuwabeba tu?elimu inachezewa na itacheza kweli nadhani huu ungekuwa wakati mzuri wa wizara ya elimu kuboresha mazingira ya elimu kwanza, wakimaliza ndo wafikirie maswala ya kupunguza ama kuongeza.Maswala ya elimu ni maswala nyeti elimu ya miaka ya kwanzia miaka ya elfu mbili na nane si ka ya miaka ilopita, elimu ilikuwa inapanda ila kwasasa elimu inasuasua, Tatizo ni wizara, serikali, walimu, muda,wazazi ama ni nini? kwa haya yote nadhani serikali inatakiwa ianze kuingilia wizara hasa inapokuwa inafanya maamuzi yenye mashaka kwa vizazi vya leo na kesho, wizara ya elimu inapaswa ishirikishe wadau kabla ya kufanya maamuzi ambayo ni mazito ka haya ya kuongeza madaraja ya ufaulu.Mwanafunzi akipata wastani wa chini ya 19 ndo anadaraja sifuri, kweli kwa mwanafunzi alokaa darasani miaka 4 anapaswa kuwekewa kiwango kidogo hivyoo? tunalengo la kufurahishana ama kufanya nini?Wito wnangu kwa wizara ya elimu ni kuondoa huo mpango wao na kuendelea na mpango wa awali huku wakiboresha mazirira ya ufundishaji na uboreshaji wa maisha ya waalimu wote.
No comments:
Post a Comment