Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Zelothe Stephen |
Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma limemkamata mtu mmoja, aliyefahamika kwa jina
la MWANGA S/O MSEMAKWELI mwenye umri wa miaka 41, Mkulima, Mkazi wa
Ising’ht kwa tuhuma za kulima Bhangi katika shamba lake.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Zelothe Stephen alisema tukio hilo
lililotokea tarehe 14/06/2012 majira ya saa 09:00 asubuhi katika kijiji
cha Insig’ht Wilaya ya Mpwapwa Mkoni Dodoma, baada ya Jeshi la Polisi
kupitia Mkakati wa Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kupokea taarifa
toka kwa wanakijiji wema kuwa kuna mtu analima bangi katika shamba lake.
“Mkulima
huyo wa bangi alikuwa amelima mazao ya Mahindi na Alizeti pembezoni
kulizunguka shamba lake na katikati alilima bangi ili kufanya
wanakijiji wenzake wasimgundue kuwa analima bangi.” Alisisitiza Kamanda
Zelothe
Bw.
Zelothe Stephen alisema iliwashangaza wanakijiji na wakulima wenzake
kuona wao wamevuna mazao yao katika mashamba yao lakini mwenzao alikuwa
hajavuna, hivyo kumtilia shaka na kumfuatilia na hatimaye kutoa taarifa
Polisi ambao walikwenda kumkamata.
Mkuu
huyo wa Polisi Mkoa wa Dodoma alisema baada ya Jeshi la Polisi kupata
taarifa hizo, walijipanga na kwenda kumkamata mtuhumiwa na kisha
kumpekua nyumbani kwake na kumkuta na kete kumi na tisa za bangi
pamoja na bangi iliyokuwa haijasokotwa ikiwa kwenye mfuko wa Nailon
ambapo ilipopimwa ilikutwa ni gram mia tano.
Aidha
Bw. Zelothe alisema Jeshi la Polisi Wilayani Mpwawa kwa kushirikiana
na wanakijiji cha insig’ht Walifanikiwa kuliteketeza kwa moto shamba
hilo la bangi lenye ukubwa wa hekali mbili.
Kamanda
Zelothe Stephen alitoa wito kwa wakulima kuacha kulima zao hilo la
bangi kwani ni kinyume na sheria za nchi na kuahidi kwamba mkulima
yeyote atakayegundulika kulima zao hilo, hatua kali na za kisheria
zitachukuliwa dhidi yake.
Wakati
huo huo Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma alisema mtu mmoja
aliyejulikana kwa jina la Allen s/o Kibwana mwenye umri wa miaka (44)
Mgogo, mkulima mkazi wa kitongoji cha mbande madukani, kata ya sajeli
tarafa ya kongwa na wilaya ya kongwa amekutwa amejinyonga nyumbani
kwake.
Kamanda
Zelothe Stephen alisema tukio hili litokea jana tarehe 15/06/2012
majira ya 06:00 asubuhi, ambapo mtu huyo alikutwa amejinyonga kwa
kutumia kamba ya katani.
Bw.
Zelothe Stephen alisema marehemu ameacha ujumbe wa barua ukieleza
kuwa sababu ya kujinyonga kwake kuwa ni mizozo ya muda mrefu na mkewe
na ndugu zake akiwatuhumu kupanga njama za kummaliza ki mapato.
No comments:
Post a Comment